Abstract:
Matamasha ya shule na vyuo nchini Kenya huandaliwa kila mwaka kati ya Januari na
Aprili. Matamasha haya hushirikisha kila shule na vyuo vya serikali pamoja na vya
binafsi. Matamasha haya yalianzishwa mwaka wa 1959. Huu ulikuwa wakati wa ukoloni
na kwa sababu hii, maigizo yalitawaliwa na sifa za matamasha na maigizo ya Uingereza
yaliyoshirikisha taasisi za elimu ya juu. Matamasha ya mwanzo mwanzo nchini Kenya
yalishirikisha taasisi za Wazungu na Wahindi pekee. Baada ya uhuru, matamasha haya
yalianza kushirikisha shule na taasisi za Kiafrika. Ingawaje lugha za Kiafrika
zimekubaliwa kushirikishwa katika tungo za kuwasilishwa katika matamasha haya,
mawasilisho mengi huwa katika lugha ya Kiingereza. Hali hii imewacha Kiswahili na
lugha nyingine za Kiafrika zikikosa kushirikishwa kikamilifu. Makala basi inajadili
nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa taifa kupitia kwa matamasha haya.
Description: